Jumamosi 19 Julai 2025 - 16:04
Yanayojiri nchini Syria ni hatari sana kwa Syria na kwa ukanda wote

Hawza / Sheikh Ali al-Khatib amegusia matukio ya hivi karibuni nchini Lebanon na katika eneo zima, hasa yanayoendelea Syria, na kusema: Yanayojiri nchini Syria ni hatari sana kwa Syria na kwa ukanda wote.

Kwa mujibu wa ripoti ya kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Hujjat al-Islam wal-Muslimin Sheikh Ali al-Khatib, Makamu wa Rais wa Baraza Kuu la Kiislamu la Kishia la Lebanon, katika ziara yake kwa mwanahistoria mashuhuri Saadoun Hamadeh nyumbani kwake huko ‘Aynu al-Tineh, alisisitiza kuwa Waislamu wa Kishia katika historia yao hawajawahi kuwa na mpango wowote wa kisiasa wa kipekee. Bali daima wamekuwa wakiuunga mkono umoja wa kitaifa, wa Kiarabu na wa Kiislamu, na wamekuwa wakiunganisha Umma juu ya yale yanayodhamini ustawi na maslahi yake. Hawajawahi kuutangazia vita upande wowote ule, bali daima wamekuwa katika hali ya kujihami.

Aligusia matukio ya hivi karibuni nchini Lebanon na katika ukanda wote, hasa matukio ya Syria, na kusema: Yanayojiri nchini Syria ni hatari sana kwa Syria na kwa ukanda wote.

Sheikh al-Khatib alieleza wazi kuwa: Mvutano unaoendelea Syria ni hatari inayokaribia, na kuingilia waziwazi utawala wa Kizayuni (Israel) katika matukio hayo ni unyang'anyi wa kijinai unaotumiwa na uadui, jambo ambalo linaweka hatari kubwa mbele ya Umma mzima, hasa kwa taifa ndugu la Syria.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha